KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Saturday, December 29, 2012

KHERI YA MWAKA MPYA 2013

Timu ya Mwanza Eagles iliyonamakazi yake kilimahewa kiloleli ,jijini mwanza, inawatakia watu wote na wachezaji wake pia kheri ya mwaka mpya wenye mafanikio mema. Inawaomba wachezaji wake waweze kujitahidi kufanya mazoezi kwa bidii ili wafike katika hali nzuri ya kiwango kinachotakiwa kimataifa. Inawaomba pia watu mbalimbali waweze kufanya kazi kwa bidii kwa mwaka ujao ili wapate kunufaika vyema na kazi yao na pesa watakazozipata.Kila la kheri kwa kila mmoja na mungu awabariki vyema mwaka 2013

Thursday, December 27, 2012

MECHI YA FUNGA NA FUNGUA MWAKA

UWANJA WA MWANZA EAGLES ULIOPO KILIMAHEWA KILOLELI AMBAPO, PATATIMKA KIVUMBI SIKU YA TAREHE 31/12/2012

BAADHI YA WACHEZAJI WA MWANZA EAGLES

Hii ni taarifa na habari nyingine tena kwa washabiki na wachezaji wa mwanza eagles ambapo patakuwa na mechi ya kufunga na kufungua mwaka,ambayo itafanyika tarehe 31/12/2012 siku ya jumatatu.Mechi hiyo inategemewa kuwa kali zaidi kutokana na mechi iliyopita dhidi ya wachezaji wa zamani(ANALOGIA) na wachezaji wasasa(DIGITAL), hivyo basi kila mmoja anashahuku na mechi hiyo huku kila mchezaji akiwa amemkamia mchezaji mwenzake. Mungu bariki mechi hiyo ili iweze kufanyika salama salmini pasipo na watu kuumizana,AMEN.

Kauli mbiu ni:  Eeeaaglleeeeeeeeeeessssssss...................HHOOOOOOOOOOOOOOTTT

Sunday, December 23, 2012

WACHEZAJI WAKIWA MAZOEZINI

Kila timu haiwezi kuwa bora na nzuri bila yakuwa na mazoezi ,wachezaji wa mwanza eagles wakiwa uwanjani kwao wanajufua vyema na mazoezi kama wanvyoonekana pichani








MECHI KATI YA WACHEZAJI WAZAMANI NA WASASA

Tarehe 22-12-2012 siku ya Jumamosi, Ni siku ambayo imewekwa rekodi ya aina yake baada ya MWANZA EAGLES TEAM kufanya mgawanyo wa wachezaji wa timu hiyo na kupata timu mbili ambazo ni timu ya wachezaji wazamani (ANALOGY) na timu ya vijana wa sasa (DIGITAL) . Mechi hiyo imechezwa katika kiwanja cha nyumbani kwao kilimewa kiloleli. Mechi hiyo ilianza kwenye mida ya sa10 jioni ambapo yimu ya ANALOGY ilikuwa ikiongozwa na mwalimu wao wa timu hiyo AMINI MUSIRA , huku timu ya DIGITAL ikiongozwa na captain wao JOHN WAMBELEGE. 

Kama ilivyo kawaida kwa maneno ya waswahili kuwa cha kale dhahabu, ndivyo hivo ilivyotokea katika mechi hiyo baada ya wachezaji wa digital kutoonesha makali yao kwa wazee hao na kujikuta wakikubali kichapo cha mabao 43 kwa 25 . Mechi hiyo ilikuwa ni ya vuta nikuvute japo timu ya Analogy waliweza kupata ushindi mkali kwa njia ya first break kupitia kwa mchezaji wao FRANCISKO MARCK .Hakika mechi hii itakuwa ya ukumbusho na ya furaha kwa wachezaji wote wa Mwanza Eagles na washabiki wake katika timu yao. Hivyo ndivyo ambavyo ilivyotokea katika mechi hiyo kwa siku ya jana jumamosi.

Thursday, December 20, 2012

MWISHO WA MWAKA 2012

Kuelekea mwisho wa mwaka wa 2012,baadhi ya wachezaji wa timu ya MWANZA EAGLES walikuwa katika harakati za kujadili kuhusu suala zima la kuwa na mechi kali yakufunga mwaka . Mechi hii huenda ikawepo siku moja au mbili , kabla ya mwaka mpya . na mechi hii itachezwa katika uwanja wao wa kilimahewa kiloleli,jijini mwanza.

Mmoja wa wachezaji hao wa mwanza eagles KHAMIDU ambae alitoa wazo hilo la kuwepo kw mchezo huo,walikuw wakitaka mechi hiyo kuwepo muda wa usiku japo mmoja wa wachezaji CHALII alicomment kwa kusema ,lazima paitajike Genereta kwa ajiri ya taa za usiku. Mpaka sasa maafikiano bado hayajakamilika japo kila mchezaji anatamani mechi hiyo iwepo kwa siku hiyo.