Timu ya mkoa wa shinyanga (Risasi) iliitembelea Club ya mwanza eagles jana kwa ajil ya kucheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa Mwanza Eagles uliopo kiloleli. Hii ni mara ya pili sasa timu hizo mbili zikikutana,kwani mara ya kwanza zilikutana mkoani shinyanga kwa mechi ya kirafiki na Mwanza Eagles akiwa mgeni na hii ni mara ya pili ambapo Risasi akiwa ni mgeni na katika mechi zote hizo timu ya Risasi inajikuta ikipoteza mechi zote . Mechi ya jana Mwanza Eagles iliishinda Risasi kwa #vikapu_66_kwa_49 na leo asubui timu ya Risasi itakwenda kucheza na timu ya Worious katika uwanja wa St.Augustin huko malimbe jijini mwanza.
Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solkjaer akiri kwamba sio rahisi kutinga
nne bora EPL
-
Manchester United inahitaji kushinda mechi tano mfululizo kati ya sita
zilizosalia ili kuweza kumaliza katika nafasi nne za kwanza katika ligi ya
Uingereza...
5 years ago
0 comments:
Post a Comment