KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Sunday, December 23, 2012

MECHI KATI YA WACHEZAJI WAZAMANI NA WASASA

Tarehe 22-12-2012 siku ya Jumamosi, Ni siku ambayo imewekwa rekodi ya aina yake baada ya MWANZA EAGLES TEAM kufanya mgawanyo wa wachezaji wa timu hiyo na kupata timu mbili ambazo ni timu ya wachezaji wazamani (ANALOGY) na timu ya vijana wa sasa (DIGITAL) . Mechi hiyo imechezwa katika kiwanja cha nyumbani kwao kilimewa kiloleli. Mechi hiyo ilianza kwenye mida ya sa10 jioni ambapo yimu ya ANALOGY ilikuwa ikiongozwa na mwalimu wao wa timu hiyo AMINI MUSIRA , huku timu ya DIGITAL ikiongozwa na captain wao JOHN WAMBELEGE. 

Kama ilivyo kawaida kwa maneno ya waswahili kuwa cha kale dhahabu, ndivyo hivo ilivyotokea katika mechi hiyo baada ya wachezaji wa digital kutoonesha makali yao kwa wazee hao na kujikuta wakikubali kichapo cha mabao 43 kwa 25 . Mechi hiyo ilikuwa ni ya vuta nikuvute japo timu ya Analogy waliweza kupata ushindi mkali kwa njia ya first break kupitia kwa mchezaji wao FRANCISKO MARCK .Hakika mechi hii itakuwa ya ukumbusho na ya furaha kwa wachezaji wote wa Mwanza Eagles na washabiki wake katika timu yao. Hivyo ndivyo ambavyo ilivyotokea katika mechi hiyo kwa siku ya jana jumamosi.

0 comments:

Post a Comment