Picha kati ya timu ya Eagles na Risasi huko Shinyanga siku ya jana
Siku ya jana jumamosi ilikuwa ni siku ambayo Timu ya Mwanza Eagles iliharikwa na Timu ya mkoa wa Shinyanga ( Risasi ) huko Shinyanga ili kuweza kucheza mechi ya kirafiki.
Safari hiyo ilipangwa vyema wiki moja kabla na siku ya jana ndio ilikuwa ni siku yenyewe ya timu hizo kukutana na kucheza mechi hiyo ya kirafiki huko Shinyanga. Mwanza Eagles ilisafiri kwenda Shinyanga siku ya jana asubuhi na baada ya mechi walifanikiwa kurudi jioni ya jana salama.
Mechi hiyo ilianza majira ya saa 10 jioni ambapo hadi mechi hiyo inamalizika timu ya Mwanza Eagles iliweza kuibuka bingwa kwa kuifunga Risasi kwa vikapu 67 kwa 61. Baada ya hapo Eagles ilianza kujiandaa kuweza kurudi Mwanza. Mechi ilienda vizuri na kila mmoja aliifurahia. Eagles wanaendelea kutoa makucha yao kwa kuendeleza ushindi katika Club yao kwa kila mechi wanayokutana nayo kwa kipindi hiki.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa siku ya jana katika mechi kati ya Risasi na Eagles huko Mkoani Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment