KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Sunday, May 25, 2014

ANGALIA MATUKIO YALIYOJILI SIKU YA JANA KWENYE MECHI YA RISASI NA EAGLES HUKO SHINYANGA









Wachezaji wa Mwanza Eagles wakiwa kwenye gar wakielekea Shinyanga
 Wachezaji wa wakiwa wamefika salama mkoani Shinyanga
 Wachezaji wakipata chakula muda mfupi baada ya kufika mkoani Shinyanga
Baada ya chakula wachezaji walienda uwanjani na kuanza kufanya zoezi dogo kabla ya mechi kuanza
Muda wa mechi ukafika na ukawa kama ambavyo ilivyo katika picha
Baadhi ya washabiki walioweza kuhudhuria mechi hiyo siku ya jana.

Wachezaji wa timu ya Risasi 
 
Hadi kufika mwisho wa mechi Eagles ilikuwa imeibuka mabingwa kwa vikapu 67 kwa 61
Na hii ndio iliyokuwa picha wa pamoja yenye kuonesha umoja,ushirikiano na upendo baina ya timu hizo mbili na ujirani mwema kati ya mkoa wa Shinyanga na jiji la Mwanza.

MWANZA EAGLES YAISHINDA TIMU YA MKOA WA SHINYANGA (RISASI)

Picha kati ya timu ya Eagles na Risasi huko Shinyanga siku ya jana

Siku ya jana jumamosi ilikuwa ni siku ambayo Timu ya Mwanza Eagles iliharikwa na Timu ya mkoa wa Shinyanga ( Risasi ) huko Shinyanga ili kuweza kucheza mechi ya kirafiki.
Safari hiyo ilipangwa vyema wiki moja kabla na siku ya jana ndio ilikuwa ni siku yenyewe ya timu hizo kukutana na kucheza mechi hiyo ya kirafiki huko Shinyanga. Mwanza Eagles ilisafiri kwenda Shinyanga siku ya jana asubuhi na baada ya mechi walifanikiwa kurudi jioni ya jana salama. 
Wachezaji wakiwa kwenye gari wakielekea Shinyanga
 
Mechi hiyo ilianza majira ya saa 10 jioni ambapo hadi mechi hiyo inamalizika timu ya Mwanza Eagles iliweza kuibuka bingwa kwa kuifunga Risasi kwa vikapu 67 kwa 61. Baada ya hapo Eagles ilianza kujiandaa kuweza kurudi Mwanza. Mechi ilienda vizuri na kila mmoja aliifurahia. Eagles wanaendelea kutoa makucha yao kwa kuendeleza ushindi katika Club yao kwa kila mechi wanayokutana nayo kwa kipindi hiki.
 
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa siku ya jana katika mechi kati ya Risasi na Eagles huko Mkoani Shinyanga.

Wednesday, May 21, 2014

ANGALIA PICHA ZA WACHEZAJI WA MWANZA EAGLES WALIPOKUWA ZIARANI GEITA (GGM)

Wakiwa ndani ya gari wakianza safari ya kwenda Geita

Wakiwa kivukoni busisi wakisubiri Ferry kwa ajili ya kwenda geita
Wakiwa ndani ya Ferry wakielekea Geita
Wakiwa wamepumzika baada ya kupokelew na wenyeji wao
Wakipata chakula
Wakiwa nje ya mgodi wa GGM mkoani Geita
Wachezaji wa Timu ya mpira wa kikapu Mjini Geita

Wachezaji wa timu ya mgodi wa GGM Mkoani Geita



                                          Wachezaji wa GGM wakiwa katika mazungumzo
Mwanza Eagles wakiwa katika picha ya pamoja


Picha ya pamoja kati ya timu ya GGM ,Geita Mjini na Mwanza Eagles
 
Ziara ya Mwanza Eagles ilifanyika siku ya jumamosi ambapo timu ya Mwanza Eagles walifanikiwa kwenda na kurudi siku hiyohiyo. Eagles Iliarikwa na timu ya Geita mjini kwenda kucheza pamoja na timu ya Geita Gold Mining(GGM) katika kiwanja kilichopo ndani ya mgodi huo. Ziara hiyo ilikuwa nzuri na yakuvutia kwani timu zote zilifurahia uwepo wa kila timu kuwepo kwa siku hiyo na timu zote zilicheza kwa muda wake tofauti,japo mvua iliharibu shuhuri hadi kufikia hatua mechi zote kuweza kuhairishwa kwasababu ya mvua.
 
Vilevile wachezaji wa Eagles waliweza kufurahia zaidi kuweza kutembelea mgodi wa GGM kwani wengi wao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kutembelea Geita na kuingia katika mgodi huo kwani walijifunza vingi na kuona mgodi ulivyo na uendeshaji wa shughuri zake pia.