KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Friday, January 31, 2014

KWA USHAURI NA MAONI WAWEZA KUTUTUMIA UJUMBE WAKO KWETU

                                       KWA BARUA PEPE WASILIANA NASI KUPITIA,

                                                                P.O BOX 2398,
                                                                 MWANZA,
                                                                 TANZANIA.


                                          KWA EMAIL WASILIANA NASI KUPITIA,
                                                
                                                ekamamusira2005@yahoo.com

VIJANA WAKIJIFUA KWA AJILI YA MECHI YA JUMAMOSI YA TAREHE 1 MWEZI 2


Monday, January 27, 2014

WACHEZAJI WA MWANZA EAGLES WAKIMBIA KIKAO AKIONGOZWA NA KOCHA MSAIDIZI FRANSIS MARCK


 Kocha wa Mwanza Eagles Amin Musira akiwa na baadhi ya wachezaji wa Mwanza Eagles wakiwa wanawasubiria wachezaji wengine wafike bahati mbaya hawakuweza kutokea

Siku ya juzi JUMAMOSI ilikuwa ni siku ambayo wachezaji wa Mwanza Eagles walitakiwa kufanya kikao kinachowahusu wao na mambo yao ya kimchezo hususa ni kuhusu kalenda nzima ya mwaka 2014 itakavyokuwa na kujadili katiba ya timu yao . Katika kikao hicho ambacho kilitakiwa kuanza majila ya sa9 alasiri, na mpaka kufikia muda wa saa 10:30 jioni wachezaji baadhi hawakuweza kuonekana hali ambayo ilimfanya Kocha mkuu AMIN MUSIRA kuduwaa na kushangaa kuwa nikwanini hadi kufikia muda huo wote wachezaji wasiweze kuonekana.

 Hadi kufikia muhafaka wa kuhairisha kikao hicho,wachezaji waliokuwa wamehudhuria ni pamoja na Kocha mkuu AMIN MUSIRA, HENRY , GERLAD , MRUSHI , BENJAMIN NA ANDREW . Hadi wachezaji hao pamoja na kocha wao walipoamua kuondoka katika sehem ya kikao ,baadhi ya wachezaji ambao hawakuweza kuonekana katika kikao hicho ni pamoja na Kocha msaidizi FRANSIS MARCK, Captain wa timu Chris, Mwasibu wa timu Paul pamoja na wachezaji wengine ambao hawakuweza kufika. Hivyo ndivyo ilivyokuwa siku hiyo ya jana ambapo wachezaji walikimbia kikao na kutoonekana kabisa.

Sunday, January 26, 2014

ST.FRANCIS YAIBUKA NA UBINGWA DHIDI YA MWANZA EAGLES KWENYE MECHI YA MARUDIANO

Big Mjula na Bobo,wote wa St.Francis

 Mechi ya marudiano dhidi ya Mwanza Eagles na St.Francis ilichezwa Ijumaa ya juzi katika uwanja wa St.Francis uliopo maeneo ya Nera katika kanisa la Nyakahoja. Mechi hiyo ilihudhuliwa na watu wachache japo mechi hiyo ilichezwa vyema. Hadi mechi inamalizika St.Francis iliibuka mabingwa kwa vikapu 60 kwa 56. Hayo ndio yaliyokuwa matokeo ya mechi hiyo dhidi ya timu hizo mbili kwa siku hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa St.Francis wakisikiliza kinachozungumzwa baada ya mechi kuisha

 Wachezaji na wapenzi wa kikapu wakisikiliza mawaidha kwa pamoja baada ya mechi kuisha 

Paul na Chris wote wa Mwanza Eagles

Chris,Gerlad na Mrushi wa Mwanza Eagles pembeni ni Jamal wa St.Francis

wachezaji wa Mwanza Eagles wakizungumza 

Baada ya mechi kuisha wachezaji wa Mwanza Eagles walibaki na kuendelea kuzungumza yakwao na hatimaye siku ikaisha.

Thursday, January 23, 2014

MWANZA EAGLES YAFUNGWA NA TIMU YA DOLPHIN


 Kama ilivyo kawaida kwa Mwanza Eagles kutafuta timu mbalimbali za kucheza nazo kirafiki, siku ya jana jumatano ilifanikiwa kwenda ugenini na kucheza mechi dhidi ya watani wao wajadi Dolphin yenye maskani yao B.O.T PASIANSI . Mechi hiyo ilichezwa Pasiansi kwenye uwanja wa timu ya Dolphin, Mechi hiyo ya jana ilikuwa ni nzuri na yenye kuvutia kwani kila mtu aliweza kuikubali kutokana na speed na wachezaji wote kuonana kwa umakini. Hadi mechi hiyo inakwisha Dolphin waliweza kuibuka kidedea dhidi ya maasimu wao wakubwa Mwanza Eagles kwa vikapu 78 kwa 64.

MWANZA EAGLES YAICHAPA ST.FRANSIS VIKAPU 62 KWA 57

MWANZA EAGLES

Katika kudumisha urafiki na undugu katika mchezo wa kikapu jijini Mwanza,timu ya Mwanza Eagles iliikaribisha timu ya St.Fransis katika uwanja wao wa kiloleli kwa ajili ya mechi. Mechi hiyo ilichezwa huku kila timu ikihitaji ubingwa huku Mwanza Eagles ikilinda heshima ya uwanja wao. Mechi hiyo ilimalizika huku Mwanza Eagles ikiwachapa St. Fransis vikapu 62 kwa 57 na kufanya matokeo hayo kuwaweka Mwanza Eagles kuwa mabingwa katika mechi hiyo.

Inatarajiwa kuwa timu ya Mwanza Eagles itaifuata timu ya St. Fransis katika uwanja wao wao uliopo kanisani Nyakahoja maeneo ya Nera jijini Mwanza.

TIMU DIGITAL YAICHAPA TIMU ANALOJIA KWA VIKAPU 54 KWA 40

Timu ya Mwanza Eagles ni timu ambayo kila mwaka huwa ikiandaa mechi nyingi zenye kuleta changamoto kubwa katika uwanja wao wa kiloleli uliopo jijini Mwanza. Hivyo katika mechi hizo huwa panakuwepo na wachezaji wengi ambao kwa asilimia kubwahurudi majumbani kwa rikizo na wanapopata fursa ya kurudi katika Club yao ya Mwanza Eagles huwa wanakutana na mechi za kuwapima uwezo wao na kufurahia kuwapo na wenzao ambao hawakuonana kwa muda mrefu.

Mechi ya Digital na Analojia ni mechi ambayo inawagawanisha wachezaji ambao ni wachezaji wa muda mrefu (wazamani amabao ni Analojia) na wachezaji wa sasa(Digital) wa Mwanza Eagles,hivyo kila mwishoni mwa mwaka mechi hii huchezwa . Kwa mwaka huu 2013 mechi hii ilichezwa na Digital walikuwa mabingwa kwenye mechi hiyo kwa vikapu 54 kwa 40 dhidi ya Analojia. 

Majina ya wachezaji wa timu hizo zilikuwa kama hivi:
Analojia
1.Gerlad
2.Ticha Amini
3.Fransis
4.Henry
5.Peter
6.Big Joachim

Digital
1.Ally
2.Chris
3.John
4.Salim
5.Hamidu
6.Shaban
7.Vicent
8.Azizi
9.Mrushi
10.Wiliam

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika mechi hii na yaliyojili. Mechi hii inatarajiwa kufanyika tena mwaka 2014 mwezi wa 12.