KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Monday, January 27, 2014

WACHEZAJI WA MWANZA EAGLES WAKIMBIA KIKAO AKIONGOZWA NA KOCHA MSAIDIZI FRANSIS MARCK


 Kocha wa Mwanza Eagles Amin Musira akiwa na baadhi ya wachezaji wa Mwanza Eagles wakiwa wanawasubiria wachezaji wengine wafike bahati mbaya hawakuweza kutokea

Siku ya juzi JUMAMOSI ilikuwa ni siku ambayo wachezaji wa Mwanza Eagles walitakiwa kufanya kikao kinachowahusu wao na mambo yao ya kimchezo hususa ni kuhusu kalenda nzima ya mwaka 2014 itakavyokuwa na kujadili katiba ya timu yao . Katika kikao hicho ambacho kilitakiwa kuanza majila ya sa9 alasiri, na mpaka kufikia muda wa saa 10:30 jioni wachezaji baadhi hawakuweza kuonekana hali ambayo ilimfanya Kocha mkuu AMIN MUSIRA kuduwaa na kushangaa kuwa nikwanini hadi kufikia muda huo wote wachezaji wasiweze kuonekana.

 Hadi kufikia muhafaka wa kuhairisha kikao hicho,wachezaji waliokuwa wamehudhuria ni pamoja na Kocha mkuu AMIN MUSIRA, HENRY , GERLAD , MRUSHI , BENJAMIN NA ANDREW . Hadi wachezaji hao pamoja na kocha wao walipoamua kuondoka katika sehem ya kikao ,baadhi ya wachezaji ambao hawakuweza kuonekana katika kikao hicho ni pamoja na Kocha msaidizi FRANSIS MARCK, Captain wa timu Chris, Mwasibu wa timu Paul pamoja na wachezaji wengine ambao hawakuweza kufika. Hivyo ndivyo ilivyokuwa siku hiyo ya jana ambapo wachezaji walikimbia kikao na kutoonekana kabisa.

0 comments:

Post a Comment