KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Friday, August 22, 2014

MECHI YA UFUNGUZI WA UWANJA WA MWANZA EAGLES JUMAMOSI ILIYOPITA

Baada ya uwanja wa mwanza eagles kukamilika,palikuwapo na mechi ya ufunguzi wa uwanja ambao ilichezwa mechi kati ya wachezaji waliochezea eagles kwa kipindi kirefu hadi hivi sasa (analojia) vs wachezaji walioichezea eagles kwa muda mchache na hadi hivi sasa wapo eagles (digital) . Mechi hiyo ilichezwa jumamosi ya wiki iliopita na hadi mechi inakwisha DIGITAL waliweza kuibuka mabingwa kwa vikapu 74 kwa 71. Na hadi hapo uwanja ukawa umefunguliwa rasmi na hivi sasa wachezaji wa mwanza eagles wapo mazoezin toka jumatatu ya wiki hii wakijifua kwa ajili ya mechi za kirafiki na mechi za hivi karibuni.
 
TEAM : Eagles Analojia
 
TEAM :Digital

Mambo yalivyokuwa uwanjani



 
Washabiki hawakutaka kupitwa mechi hii



Na huyu ndiye refferee aliyechezesha mechi hiyo...anajulikana kwa jina la COACH BENSON

UWANJA WA MWANZA EAGLES WAKAMILIKA KUJENGWA

Muonekano mpya wa uwanja wa mwanza eagles
Uwanja wa mwanza eagles ulianza kufanyiwa marekebisho mwishoni mwa mwezi wa6,hadi kufikia tarehe 10 mwezi huu ,uwanja ulikuwa tayar umekamilika. Wachezaji waliweza kujitolea kwa moyo mkunjufu kuweza kusimamia na kusaidia shughuri zilizokuwa zikiendelea katika ujenzi hadi kukamilika kwa uwanja huo hakika wanahitaji pongezi kwani haikuwa kazi rahisi.

Uwanja huo ulioko maeneo ya kilimahewa kiloleli jijini mwanza,umeweza kufanikishwa kwa namna moja au nyingine na mwalimu wa Club hiyo aitwae AMIN MUSIRA , na anaitaji kupew pongezi kubwa sana amefanya kitu cha muhimu na chenye manufaa katika mchezo wa mpira wa kikapu hapa jijini mwanza.Mwalimu huyo ndie aliyeweza kutafuta wadhamini na kumsaidia kufanya kitendo hicho cha kujenge na kurekebisha uwanja huo.Katika jiji la mwanza ni club moja tu ya mwanza eagles iliyonauwanja wake na ndicho kiwanja ambacho ni bora kuliko viwanja vyote vilivyopo jijini mwanza na kanda ya ziwa pia.
Uwanja huu unasehemu za watu kukaa huku mechi au mazoezi yakiendelea

Baada ya uwanja huo kuwa umekamilika, ilibidi ufanyiwe ufunguzi wa kuufungua uwanja huo rasmi kwa mazoezi na mechi pia. Uwanja huo uliweza kufunguliwa kwa kuandaa Mechi ambayo ilichezwa jumamosi ya wiki iliyoisha. mechi hiyo ilikuwa ni kati ya wachezaji walioichezea club ya mwanza eagles kwa muda mrefu (analojia) na wachezaji ambao hawana muda mrefu wakiichezea club ya eagles (digital) . mechi mechi hiyo ilichezwa na hadi kufikia tamati Digitali iliishinda Analojia kwa vikapu 74 kwa 71.

wachezaji wa mwanza eagles sasa wapo mazoezini tangu jumatatu baada ya kutokuwa na mazoez mwezi mzima na kujikuta wakifanya vibaya katika ligi ya crossover sasa wanajifua upya kimazoezi.


Wednesday, July 16, 2014

TAZAMA PICHA ZA UWANJA WA MWANZA EAGLES UKIJENGWA


Kocha wa timu ya Mwanza Eagles AMIN MUSIRA wa pili kutoka kulia akiwa ameegemea pipa ,akiwa na wachezaji wake wakizungumza 

Baadhi ya wachezaji wa Mwanza Eagles wakiwa na moja ya wapenzi wa Club hiyo katika picha. Kuanzia kulia ni Ally, Frank, Erick, Kerlvin, Gerald, Benny na Sweetbert
Hivi ndivyo uwanja unavyoonekana upande mmoja

UJENZI WA UWANJA WA BASKETBALL WA MWANZA EAGLES WAANZA RASMI.

Mwanza Eagles Basketball Club yenye maskani yake kiloleli kilimahewa jijini Mwanza, Club hiyo ilikuwa katika mikakati ya kurekebisha uwanja wao ambao ulikuwa ukionesha hali ya kuchakaa kwa muda mrefu. Na hadi kufikia Jumamosi ya wiki iliyopita uwanja huo ulianza kurekebishwa kwa sehemu baadhi na jumapili ndio iliyokuwa siku ambayo uwanja ulianza kurekebishwa rasmi.

Uwanja huo unatakribani miaka mitano sasa toka urekebishwe kwa kiwango kinachoonekana kwa kipindi hichi. Hivyo sasa,muda huu umekuwa ni muafaka kuweza kuurekebisha tena na kuweza kurudia hali yake ya awali na wenye hadhi ya kisasa. Marekebisho ya sasa ni kuweka sakafu ingine yenye hadhi ya kitofauti na ile iliyokuwepo,ulekebishwaji wa magori pamoja na board za gori, uwekwaji wa sehemu ya washabiki kukaa pamoja na officials. Urekebishwaji wa uwanja huo utaweza kuchukua muda wa mwezi mzima hadi kukamilika kwa marekebisho hayo.

Wachezaji na wanachama wa club hiyo wapo sambamba na usimamizi na usaidizi wa ujenzi wa uwanja ikiwemo kumwagilia maji katika sakafu,pamoja na miti aliyopandwa pembeni ya uwanja huo na kazi ndogondogo ambazo wao wanaweza kuzifanya. 

Baada ya uwanja kukamilika na kuwa tayari kwa matumizi , patakuwa na mechi ya ufunguzi wa uwanja ambayo itakuwa kati ya timu ya mwanza eagles na timu ingine kutoka hapa jijini mwanza japo mpaka sasa haijatajwa kuwa ni timu ipi. Siku ya mechi ya ufunguzi patakuwa na muziki na mwaliko wa timu za basketball hapa mwanza ili kuweza kufurahia pamoja siku hiyo.
Kocha wa Club ya Mwanza Eagles,AMIN MUSIRA akiwa anawaonesha wachezaji wake namna ya kumwagilizia sakafu


Sunday, June 22, 2014

MWANZA EAGLES KUANDAA LIGI IITWAYO CROSSOVER JIJINI MWANZA

 Club ya Mwanza Eagles imeweza kufikia hatua ya kuweza kuandaa ligi ya mpira wa kikapu ambayo timu zote za Mwanza zitaweza kushiriki . Ligi hiyo inatarajiwa kuanza siku ya jumamosi tarehe 28/06 mwaka huu. Ni ligi ambayo itashirikisha timu 8 za hapa jijini mwanza ambazo kila timu itaweza kukutana na timu nyenzake kwa upande wa nyumbani na ugenini. Kila mshiriki katika kila timu atapata cheti cha ushiriki. kutakuwa na vyeti kwa wale wachezaji ambawo wataweza kufanya vizur kutokana na cartegories tofautitofauti

Timu zitakazo shiriki katika ligi.

  1. Mwanza Eagles
  2. Dolphin
  3. St. Fransis
  4. Worrious
  5. Bugando Heat
  6. Bugando College
  7. Spider
  8. Planet
Zawadi zitakwenda kwa;


  1. Timu bingwa
  2. Timu ya pili
  3. Timu ya tatu
  4. Timu with Best Movies
  5. Most displined Team
  6. Popular player
Zawadi zingne zitakwenda kwa;


  1. Best Diffender
  2. Best dunker
  3. Best playmaker
  4. Best Ringbound
  5. Fair player
  6. MVP
  7. Best shooter
  8. Best 3-pointer
  9. Up-coming player
Viwanja vitakavyotumika;


  1. Uwanja wa Mwanza Eagles
  2. Uwanja wa B.O.T Pasiansi
  3. Uwanja wa St.Augustin, Malimbe
  4. Uwanja wa Bugando Spider
Ligi hiyo itaweza kuchukua muda wa takribani mwezi mzima. Siku za mechi zitakuwa ni kuanzia siku ya Alhamisi hadi jumapili kwa kila wiki. na inatarajiwa kuwa na mechi moja kwa kila siku katika viwanja tofauttofauti. Wadau na wapenzi wa mpira wa kikapu. mnakaribishwa sana kuja kuangalia ligi hii ambayo itakuwa ikiendelea kwa muda huo wote.

MWANZA EAGLES YAIFUNGA TIMU YA SHINYANGA (RISASI) JANA JUMAMOSI


Timu ya mkoa wa shinyanga (Risasi) iliitembelea Club ya mwanza eagles jana kwa ajil ya kucheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa Mwanza Eagles uliopo kiloleli. Hii ni mara ya pili sasa timu hizo mbili zikikutana,kwani mara ya kwanza zilikutana mkoani shinyanga kwa mechi ya kirafiki na Mwanza Eagles akiwa mgeni na hii ni mara ya pili ambapo Risasi akiwa ni mgeni na katika mechi zote hizo timu ya Risasi inajikuta ikipoteza mechi zote . Mechi ya jana Mwanza Eagles iliishinda Risasi kwa #vikapu_66_kwa_49 na leo asubui timu ya Risasi itakwenda kucheza na timu ya Worious katika uwanja wa St.Augustin huko malimbe jijini mwanza.