Mwanza Eagles Basketball Club yenye maskani yake kiloleli kilimahewa jijini Mwanza, Club hiyo ilikuwa katika mikakati ya kurekebisha uwanja wao ambao ulikuwa ukionesha hali ya kuchakaa kwa muda mrefu. Na hadi kufikia Jumamosi ya wiki iliyopita uwanja huo ulianza kurekebishwa kwa sehemu baadhi na jumapili ndio iliyokuwa siku ambayo uwanja ulianza kurekebishwa rasmi.
Uwanja huo unatakribani miaka mitano sasa toka urekebishwe kwa kiwango kinachoonekana kwa kipindi hichi. Hivyo sasa,muda huu umekuwa ni muafaka kuweza kuurekebisha tena na kuweza kurudia hali yake ya awali na wenye hadhi ya kisasa. Marekebisho ya sasa ni kuweka sakafu ingine yenye hadhi ya kitofauti na ile iliyokuwepo,ulekebishwaji wa magori pamoja na board za gori, uwekwaji wa sehemu ya washabiki kukaa pamoja na officials. Urekebishwaji wa uwanja huo utaweza kuchukua muda wa mwezi mzima hadi kukamilika kwa marekebisho hayo.
Wachezaji na wanachama wa club hiyo wapo sambamba na usimamizi na usaidizi wa ujenzi wa uwanja ikiwemo kumwagilia maji katika sakafu,pamoja na miti aliyopandwa pembeni ya uwanja huo na kazi ndogondogo ambazo wao wanaweza kuzifanya.
Baada ya uwanja kukamilika na kuwa tayari kwa matumizi , patakuwa na mechi ya ufunguzi wa uwanja ambayo itakuwa kati ya timu ya mwanza eagles na timu ingine kutoka hapa jijini mwanza japo mpaka sasa haijatajwa kuwa ni timu ipi. Siku ya mechi ya ufunguzi patakuwa na muziki na mwaliko wa timu za basketball hapa mwanza ili kuweza kufurahia pamoja siku hiyo.
Kocha wa Club ya Mwanza Eagles,AMIN MUSIRA akiwa anawaonesha wachezaji wake namna ya kumwagilizia sakafu
0 comments:
Post a Comment