KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Friday, August 22, 2014

UWANJA WA MWANZA EAGLES WAKAMILIKA KUJENGWA

Muonekano mpya wa uwanja wa mwanza eagles
Uwanja wa mwanza eagles ulianza kufanyiwa marekebisho mwishoni mwa mwezi wa6,hadi kufikia tarehe 10 mwezi huu ,uwanja ulikuwa tayar umekamilika. Wachezaji waliweza kujitolea kwa moyo mkunjufu kuweza kusimamia na kusaidia shughuri zilizokuwa zikiendelea katika ujenzi hadi kukamilika kwa uwanja huo hakika wanahitaji pongezi kwani haikuwa kazi rahisi.

Uwanja huo ulioko maeneo ya kilimahewa kiloleli jijini mwanza,umeweza kufanikishwa kwa namna moja au nyingine na mwalimu wa Club hiyo aitwae AMIN MUSIRA , na anaitaji kupew pongezi kubwa sana amefanya kitu cha muhimu na chenye manufaa katika mchezo wa mpira wa kikapu hapa jijini mwanza.Mwalimu huyo ndie aliyeweza kutafuta wadhamini na kumsaidia kufanya kitendo hicho cha kujenge na kurekebisha uwanja huo.Katika jiji la mwanza ni club moja tu ya mwanza eagles iliyonauwanja wake na ndicho kiwanja ambacho ni bora kuliko viwanja vyote vilivyopo jijini mwanza na kanda ya ziwa pia.
Uwanja huu unasehemu za watu kukaa huku mechi au mazoezi yakiendelea

Baada ya uwanja huo kuwa umekamilika, ilibidi ufanyiwe ufunguzi wa kuufungua uwanja huo rasmi kwa mazoezi na mechi pia. Uwanja huo uliweza kufunguliwa kwa kuandaa Mechi ambayo ilichezwa jumamosi ya wiki iliyoisha. mechi hiyo ilikuwa ni kati ya wachezaji walioichezea club ya mwanza eagles kwa muda mrefu (analojia) na wachezaji ambao hawana muda mrefu wakiichezea club ya eagles (digital) . mechi mechi hiyo ilichezwa na hadi kufikia tamati Digitali iliishinda Analojia kwa vikapu 74 kwa 71.

wachezaji wa mwanza eagles sasa wapo mazoezini tangu jumatatu baada ya kutokuwa na mazoez mwezi mzima na kujikuta wakifanya vibaya katika ligi ya crossover sasa wanajifua upya kimazoezi.


0 comments:

Post a Comment