KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Sunday, June 22, 2014

MWANZA EAGLES KUANDAA LIGI IITWAYO CROSSOVER JIJINI MWANZA

 Club ya Mwanza Eagles imeweza kufikia hatua ya kuweza kuandaa ligi ya mpira wa kikapu ambayo timu zote za Mwanza zitaweza kushiriki . Ligi hiyo inatarajiwa kuanza siku ya jumamosi tarehe 28/06 mwaka huu. Ni ligi ambayo itashirikisha timu 8 za hapa jijini mwanza ambazo kila timu itaweza kukutana na timu nyenzake kwa upande wa nyumbani na ugenini. Kila mshiriki katika kila timu atapata cheti cha ushiriki. kutakuwa na vyeti kwa wale wachezaji ambawo wataweza kufanya vizur kutokana na cartegories tofautitofauti

Timu zitakazo shiriki katika ligi.

  1. Mwanza Eagles
  2. Dolphin
  3. St. Fransis
  4. Worrious
  5. Bugando Heat
  6. Bugando College
  7. Spider
  8. Planet
Zawadi zitakwenda kwa;


  1. Timu bingwa
  2. Timu ya pili
  3. Timu ya tatu
  4. Timu with Best Movies
  5. Most displined Team
  6. Popular player
Zawadi zingne zitakwenda kwa;


  1. Best Diffender
  2. Best dunker
  3. Best playmaker
  4. Best Ringbound
  5. Fair player
  6. MVP
  7. Best shooter
  8. Best 3-pointer
  9. Up-coming player
Viwanja vitakavyotumika;


  1. Uwanja wa Mwanza Eagles
  2. Uwanja wa B.O.T Pasiansi
  3. Uwanja wa St.Augustin, Malimbe
  4. Uwanja wa Bugando Spider
Ligi hiyo itaweza kuchukua muda wa takribani mwezi mzima. Siku za mechi zitakuwa ni kuanzia siku ya Alhamisi hadi jumapili kwa kila wiki. na inatarajiwa kuwa na mechi moja kwa kila siku katika viwanja tofauttofauti. Wadau na wapenzi wa mpira wa kikapu. mnakaribishwa sana kuja kuangalia ligi hii ambayo itakuwa ikiendelea kwa muda huo wote.

MWANZA EAGLES YAIFUNGA TIMU YA SHINYANGA (RISASI) JANA JUMAMOSI


Timu ya mkoa wa shinyanga (Risasi) iliitembelea Club ya mwanza eagles jana kwa ajil ya kucheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa Mwanza Eagles uliopo kiloleli. Hii ni mara ya pili sasa timu hizo mbili zikikutana,kwani mara ya kwanza zilikutana mkoani shinyanga kwa mechi ya kirafiki na Mwanza Eagles akiwa mgeni na hii ni mara ya pili ambapo Risasi akiwa ni mgeni na katika mechi zote hizo timu ya Risasi inajikuta ikipoteza mechi zote . Mechi ya jana Mwanza Eagles iliishinda Risasi kwa #vikapu_66_kwa_49 na leo asubui timu ya Risasi itakwenda kucheza na timu ya Worious katika uwanja wa St.Augustin huko malimbe jijini mwanza.

Thursday, June 12, 2014

TIMU YA MKOA YA MUSOMA YAIBUKA BINGWA DHIDI YA MWANZA EAGLES JUMAMOSI ILIYOPITA

Timu ya Mwanza Eagles ambayo ilikuwa na ziara yake Mkoani Musoma jumamosi ya juma lililopita,iliweza kwenda huko na kucheza na timu ya Mkoa wa Musoma, ambapo timu hiyo ilishinda kwa ubingwa wa vikapu 71 kwa 90

Baadhi ya wachezaji wa Mwanza Eagles wakiwa kwenye gari wakielekea Musoma

Wachezaji wamefika musoma

wachezaji wakipata chakula baada ya safari ndefu

wachezaji wa Mwanza Eagles

Mechi ikiendelea

Mechi iliisha na baada ya hapo picha ya pamoja ilipigwa na wote wakazidi kufahamiana