KARIBU NA TEMBELEA ZAIDI BLOG HII ILI KUPATA NA KUJUA MABO MENGI ZAIDI KUHUSU MWANZA EAGLES BASKETBALL TEAM NA MENGINEYO MENGI KUHUSU MICHEZO YA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA.

Sunday, March 30, 2014

EAGLES YAISHINDA TIMU YA GEITA KWA VIKAPU 72 KWA 28

Leo jumamosi Mwanza Eagles ilipata ugeni mkubwa baada ya timu ya mkoa wa Geita kufunga safari na kuja Mwanza kucheza mechi ya kirafiki na Mwanza Eagles. Mechi ambayo ilichezwa leo katika kiwanja cha kiloleli,kilimahewa,jijini Mwanza. Mechi hiyo ilihudhuliwa kwa wingi na baadhi ya washabiki na wapenzi wa mpira wa kikapu na kuleta hamasa kubwa kwa wachezaji na washabiki pia. Mechi hiyo ilifika tamati kwa Mwanza Eagles kuibuka mabingwa kwa kuwafunga Geita vikapu 72 kwa 28.
Kesho Eagles itakuwa ikicheza na timu ya Bugando Collage majira ya jioni katika uwanja wa kiloleli kilimahewa.
Matukio ya mechi hiyo yalikuwa kama hivi.

Fransisco( alikuwa referee katika mechi ya leo)

Officials
Timu ya Geita ikinyoosha viungo kabla ya kuanza mechi

Eagles wakizungumza kwenye time out

Geita wakizungumza
Viongozi wa timu ya Eagles na Geita

Picha ya pamoja kati ya timu ya Eagles na timu ya Geita
 





0 comments:

Post a Comment