Mechi ya EAST na West ,Ni mechi ambayo inasubiliwa kwa hamu kubwa na wachezaji wote wa Mwanza Eagles ambao kila upande unamtambia mwenzake juu ya ushindi watakao upata dhidi ya wenzao. Hii ni mechi kati ya wachezaji wa Mwanza Eagles wanaoishi upande wa East na wengine wa upande wa West mwa jiji la Mwanza . Mechi hii huwa inatokea mara moja kwa mwaka ambapo huwakutanisha wachezaji takribani wote wa Mwanza Eagles na kufanya kitu kimoja cha kipekee na kuwakutanisha ndugu ,jamaa, na wachezaji ambao hawakuweza kuonana kwa muda mrefu.
Mechi ya East na West itafanyika siku ya jumamosi tarehe 14/12/2013 katika uwanja wa kiloleli jijini Mwanza ambao ni uwanja wa Mwanza Eagles Team. Muda wa mechi hiyo itakuwa muda wa saa 10 kamili jioni ambapo inategemewa kumalizika mapema na watu kufurahia mchezo huo kwa pamoja.
Watu wote mnakaribishwa sana katika mechi hiyo, ndugu jamaa , marafiki ,wapenzi wa washabiki wa mpira wa kikapu ,mnakaribishwa kuona mechi hiyo yenye ushindani mkubwa .